Odillon Rweyendera akimvalisha pete Glory Lwomile wakati wa ibada ya ndoa iliyofanyika katika kanisa la Mt Mathias Mulumba Kalemba jimbo kuu la Songea mjini Songea na kufuatiwa na sherehe ya kuwapongeza katika ukumbi wa Familia Takatifu Bombambili.
Glory Lwomile akimvisha pete ya ndoa mume wake Odillon Rweyendera wakati wa misa iliyofanyika katika kanisa la Mt Mathias Mulumba Kalembo jimbo kuu la Songea mjini Songea.
Maharusi Odillon Rweyendera na Glory Lwomile wakiwa na furaha mara baada ya kufunga ndoa katika kanisa la Mt Mathias Mulumba Kalemba jimbo kuu la Songea mkoani Ruvuma,Bwana harusi ni mfanyakazi wa shirika la umeme nchini Tanesco mkoa wa Ruvuma na Bi Harusi ni Hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.
Maharusi Odillon Rweyendera na Glory Lwomile wakigonga cheers wakati wa sherehe ya kuwapongeza iliyofanyika katika ukumbi wa familia Takatifu Parokia ya Bombambili iliyotanguliwa na misa ya ndoa katika kanisa la Mt Mathias Mulumba Kalemba mjini Songea.
Baadhi ya ndugu na jamaa wakigonga cheers na maharusi Odillon Rweyendera na Glory Lwolime wakati wa sherehe ya kuwapongeza katika ukumbi wa Familia Takatifu Bombambili mjini Songea.
Maharusi wakikata keki.
Bwana harusi Odillon Rweyendera akimlisha kipande cha keki mkewe Glory Lwomile wakati wa sherehe ya kuwapongeza kama ishara ya upendo baada ya kufunga ndoa yao.
Viongozi wa kamati ya maandalizi ya harusi ya Odillon Rweyendera na Glory Lwomile wakifuatilia kwa karibu matukio ya sherehe ya kuwapongeza maharusi katika ukumbi wa familia Takatifu Bombambili.
Maharusi Odillon Rweyendera na Glory Lwomile wakipokea zawadi kutoka kwa kamati ya maandalizi ya harusi yao.
Baadhi ya ndugu,jamaa na marafiki wakicheza muziki na maharusi Odillon Rweyendera na Glory Lwolime, kama ishara ya furaha kwa ndugu zao kufunga ndoa takatifu.
No comments:
Post a Comment